Home » » SHEIKH OMAR MOHAMED AZUNGUMZIA MAUAJI YALIYOTOKEA HANDENI

SHEIKH OMAR MOHAMED AZUNGUMZIA MAUAJI YALIYOTOKEA HANDENI

Written By mahamoud on Wednesday, December 25, 2013 | 2:43 PM

Share this article :

1 comments:

  1. Miezi michache iliyopita vyombo vya habari vilisheheni taarifa ya magaidi waliokuwa katika vijiji vya Handeni.Taarifa zilifika Tanga kuwa kulikuwa na magaidi wanaishi katika mahandaki na operesheni maalum ilikuwa ikifanyika kuwateketeza.

    Propaganda ikaenezwa kuwa walikuwa hawaitambui serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Habari zilivuja Tanga mjini na vitongiji vyake kuwa kuna vijiji vimeteketezwa.

    Kwa hakika kuna watu waliletwa Hospitali ya Bombo wakiwa na majeraha ya risasi.

    Kwa watu waliofika Hospitali ya Bombo kwa kweli waliwaona vijana waliokuwa wamefungwa pingu wakiwa katika vitanda vyao huku wakilindwa na askari.

    Taarifa zikafika vilevile kuwa kuna watoto wadogo wamefikishwa Tanga baada ya kukutwa porini.Watoto hawa walikuwa wamehifadhiwa katika moja ya shule za hapo mjini.

    Katika hali kama hiyo vilevile zikafika taarifa tofauti kwa Waislam wa Tanga kuwa hao walioletwa Hosptali ya Bombo na watoto waliookotwa porini ni Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande walioshambuliwa na askari pasi na sababu.

    Juhudi za Umoja wa Taasisi za Kiislam Tanga (SHITA) chini ya Mayor Omari Guledi na Katibu wake Ahmed Mustafa kukutana na Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa kupata ukweli zikagonga mwamba.

    Hali ikawa tete baada ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso mmoja katika masheikh vijana mjini Tanga kukamatwa na kuwekwa rumande kisha kuhamishwa Handeni ambako alifunguliwa kesi ya kubambika ya ''kushawishi mauaji.''

    Ikavuma kuwa patakuwa na maandamano kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Chanmbuso.Askari wa FFU walizingira misikiti kadhaa Ijumaa hiyo lakini hapakuwa na maadamano yoyote.

    Alipopata dhamana na kuachiwa Sheikh Chambuso alikuja Tanga na habari za kutisha kuhusu dhulma iliyopita katika vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande.

    Habari hizi alielezwa na mahabusi wendake katika hivyo vijiji vilivyoshambuliwa.Sheikh Chambuso katika hotuba aliyotoa katika moja ya misikiti maarufu Tanga aliwafahamisha Waislam kuhusu misikiti iliyovujwa na kuchomwa moto, Qur'an zillizochoiwa moto na nyumba za Waislam zilizoteketezwa kwa kisingizo cha ugaidi.

    ReplyDelete