MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi la Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda la kufanya mapitio ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro wa kukataa kumfutia kosa la uchochezi wakati yupo kwenye kifungo cha mwaka mmoja nje.
Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Rose Temba, alisema ombi hilo limekosa thamani katika jicho la sheria.
Jaji Temba alisema Oktoba mwaka huu, mawakili wa Ponda walivyowasilisha ombi hilo kabla jalada halijapelekwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu Dar es Salaam alipata fursa ya kulipitia na kubaini upungufu kwenye hati ya kiapo.
“Nilishangaa Desemba 2 mwaka huu, wakili wa Ponda, Juma Nassoro alipinga kiapo hicho kilikuwa hakina dosari… binafsi nilipitia jalada na kuona rekodi za mahakama haziko sahihi na zilirekebishwa kinyemela baadae, kitendo hicho kinahesabika kama ni utovu wa nidhamu.
“Ukiukwaji huu hauwezi kuachwa hivi hivi bali vyombo vinavyoshughulika na nidhamu kwa mawakili nchini viwachukulie hatua mawakili wa Ponda,” alisema.
Akizungumzia hoja ya kiapo kuwa kina dosari, Jaji Temba alisema anakubaliana na pingamizi la awali la upande wa Jamhuri lililowasilishwa na Wakili Kiongozi wa Serikali, Bernad Kongora kuwa kiapo hakina tarehe na baadae kilifanyiwa marekebisho kinyemela.
“Kwa dosari hiyo ya hati ya kiapo, mahakama inakubaliana na Wakili wa Jamhuri, Kongola kuwa ombi la mapitio nalo limekosa thamani katika jicho la sheria na kwa maana hiyo mahakama inakubaliana na pingamizi la awali la upande wa Jamhuri kuwa kiapo kina upungufu,” alisema.
Desemba 2 mwaka huu, Kongora aliwasilisha pingamizi la awali akiomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwa sababu hati ya kiapo ina dosari.
Oktoba mwaka huu, Ponda aliwasilisha ombi hilo kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kukataa kumfutia kosa la uchochezi wakati yupo ndani ya kifungo cha mwaka mmoja nje ambacho kilimtaka asitende makosa na awe raia mwema.
Sheikh Ponda anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti mwaka huu mkoani Morogoro.

0 comments:
Post a Comment