Home » » MKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA KWENYE MSIBA WA MANDELA AZUSHA KIZAAZAA

MKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA KWENYE MSIBA WA MANDELA AZUSHA KIZAAZAA

Written By mahamoud on Saturday, December 14, 2013 | 6:42 AM

Photo: MKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA KWENYE MSIBA WA MANDELA AZUSHA KIZAAZAA  Wakati mamilioni ya watu duniani kote walikuwa wakifuatilia na kuvutiwa na hotuba zilizokuwa zikitolewa katika shughuli ya mazishi ya mzee Nelson Mandela, jumuiya ya kimataifa ya watu wenye ulemavu wa kusikia imeelezea kughadhibishwa kwake na kile walichosema kuwa mkalimali wa lugha ya alama aliyetumika katika shughuli hiyo alikuwa mkalimani bandia.  Kwa mujibu wa ripoti iliochapishwa kwenye mtandao wa SBS News wa Australia, mlemavu kutoka Afrika Kusini na ambaye ni mwanachama wa Tawi la Vijana la Shirikisho la viziwi duniani, Braam Jordaan, alisema kuwa mkalimani huyo alikuwa akijitengenezea alama zake mwenyewe ambazo hazipo kabisa kwenye lugha ya alama.   Jordaan anadai kuwa ishara za mikono, uso na harakati za mwili hazikuwa zikifuata kile kilichokuwa kikisemwa na mzungumzaje, na kwamba tukio hilo limetia aibu katika shughuli hiyo muhimu kwa taifa lake.   Mwakilizi wa Jumuiya ya Wakalimani wa Lugha ya Alama ulimwenguni, Sheena Walters naye pia aliuambia mtandao wa SBS kuwa harakati za mikono zilizokuwa zikitumiwa na mkalimani hazitambuliki katika aina yoyote ya lugha ya alama.  Sheena alisema kuwa lugha nyingi za alama duniani zina muundo na mfumo unaofanana na kwamba mkalimani huyo alikuwa akirudiarudia alama zilizoonekana kutofahamika au kuonekana kwa wanaomfuatili.  Wakati shughuli za mazishi zikitangazwa moja kwa moja na vyombo vingi vya habari ulimwenguni, wanachama wa jumuiya hiyo ya viziwi walimiminika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea hasira zao juu ya tukio hilo.  Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, chama tawala cha Afrika ya Kusini, ANC kimekuwa kikimtumia mkalimani huyo, na kiliwahi kulalamikiwa juu ya udhaifu wake.  (Pichani: Mkalimani wa Lugha ya Alama akiwa pembezoni mwa Rais Obama)Wakati mamilioni ya watu duniani kote walikuwa wakifuatilia na kuvutiwa na hotuba zilizokuwa zikitolewa katika shughuli ya mazishi ya mzee Nelson Mandela, jumuiya ya kimataifa ya watu wenye ulemavu wa kusikia imeelezea kughadhibishwa kwake na kile walichosema kuwa mkalimali wa lugha ya alama aliyetumika katika shughuli hiyo alikuwa mkalimani bandia.

Kwa mujibu wa ripoti iliochapishwa kwenye mtandao wa SBS News wa Australia, mlemavu kutoka Afrika Kusini na ambaye ni mwanachama wa Tawi la Vijana la Shirikisho la viziwi duniani, Braam Jordaan, alisema kuwa mkalimani huyo alikuwa akijitengenezea alama zake mwenyewe ambazo hazipo kabisa kwenye lugha ya alama.

Jordaan anadai kuwa ishara za mikono, uso na harakati za mwili hazikuwa zikifuata kile kilichokuwa kikisemwa na mzungumzaje, na kwamba tukio hilo limetia aibu katika shughuli hiyo muhimu kwa taifa lake.

Mwakilizi wa Jumuiya ya Wakalimani wa Lugha ya Alama ulimwenguni, Sheena Walters naye pia aliuambia mtandao wa SBS kuwa harakati za mikono zilizokuwa zikitumiwa na mkalimani hazitambuliki katika aina yoyote ya lugha ya alama.

Sheena alisema kuwa lugha nyingi za alama duniani zina muundo na mfumo unaofanana na kwamba mkalimani huyo alikuwa akirudiarudia alama zilizoonekana kutofahamika au kuonekana kwa wanaomfuatili.

Wakati shughuli za mazishi zikitangazwa moja kwa moja na vyombo vingi vya habari ulimwenguni, wanachama wa jumuiya hiyo ya viziwi walimiminika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea hasira zao juu ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, chama tawala cha Afrika ya Kusini, ANC kimekuwa kikimtumia mkalimani huyo, na kiliwahi kulalamikiwa juu ya udhaifu wake.

(Pichani: Mkalimani wa Lugha ya Alama akiwa pembezoni mwa Rais Obama)
Share this article :

0 comments:

Post a Comment