Home » » WAANDAMANAJI THAILAND WAZIDI KUMSHINIKIZA WAZIRI MKUU

WAANDAMANAJI THAILAND WAZIDI KUMSHINIKIZA WAZIRI MKUU

Written By mahamoud on Saturday, December 14, 2013 | 6:44 AM

Photo: WAANDAMANAJI THAILAND WAZIDI KUMSHINIKIZA WAZIRI MKUU  • Wataka ashitakiwe kwa uhaini  Waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Thailand wameendelea kumshinikiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Yingluck Shinawatra, wakisema anatakiwa kushitakiwa kwa uhaini.   Waandamanaji hao wanasema kuwa wanataka kufuta kabisa nyayo za kaka wa kiongozi huyo, Thaksin Shinawatra, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kuondolewa katika mapinduzi ya mwaka 2006. Wanadai kuwa bilionea huyo bado anaiendesha nchi kwa mlango wa nyuma.  Haya yanatokea baada ya Bi. Yingluck kuitisha uchaguzi wa mapema na kutangaza kulivunja bunge katika kujaribu kutuliza hali ya mambo nchini mwake.  Juzi kiongozi wa waandamanaji, Suthep Thaugsuban, ambaye alijiuzulu ubunge ili kuongoza maandamano, alimpa Yingluck saa 24 awe amejiuzulu.  Jana Suthep alisema kuwa polisi walitakiwa kumkamata Yingluck kwa kuwa muda wa saa 24 ulikuwa umekwisha.   "Ninawataka polisi wamakamate Yingluck kwa uhaini kwa sababu hajatekeleza maagizo yetu,” aliwaambia maelfu ya waandamanaji walioweka kambi nje ya jengo la serikali.  "Kama hutatusikiliza, tutazidisha maandamano mpaka wewe na familia yote ya Shinawatra mshindwe kutembea. Mtawezaje kutembea wakati watu wakiwatemea mate kila siku?” aliongeza.   Hata hivyo, Yingluck, alipuuza wito wa waandamanaji wa kumtaka ajiuzulu, akiapa kuendelea kuwa waziri mkuu wa mpito mpaka uchaguzi mkuu utakaofanyika Februari 2.   Maandamano ya kuipingia serikali yalianza Oktoba 31 baada ya serikali kuwasilisha bunge muswada ambao ungetoa msamaha kwa Thaksin na kumuwezesha kurejea nchini.   Waandamanaji wanamtuhumu Thaksin kuwa bado anaiendesha nchi kwa mlango wa nyuma, na wameapa kuibomoa nguvu yake katika siasa za nchi hiyo.  Bilionea huyo aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya mwaka 2006, amekuwa akiishi uhamishoni tangu mwaka 2008. Mahakama nchini humo ilimpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela iwapo atarejea Thailand. 
• Wataka ashitakiwe kwa uhaini

Waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Thailand wameendelea kumshinikiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Yingluck Shinawatra, wakisema anatakiwa kushitakiwa kwa uhaini.

Waandamanaji hao wanasema kuwa wanataka kufuta kabisa nyayo za kaka wa kiongozi huyo, Thaksin Shinawatra, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kuondolewa katika mapinduzi ya mwaka 2006. Wanadai kuwa bilionea huyo bado anaiendesha nchi kwa mlango wa nyuma.

Haya yanatokea baada ya Bi. Yingluck kuitisha uchaguzi wa mapema na kutangaza kulivunja bunge katika kujaribu kutuliza hali ya mambo nchini mwake.

Juzi kiongozi wa waandamanaji, Suthep Thaugsuban, ambaye alijiuzulu ubunge ili kuongoza maandamano, alimpa Yingluck saa 24 awe amejiuzulu.

Jana Suthep alisema kuwa polisi walitakiwa kumkamata Yingluck kwa kuwa muda wa saa 24 ulikuwa umekwisha.

"Ninawataka polisi wamakamate Yingluck kwa uhaini kwa sababu hajatekeleza maagizo yetu,” aliwaambia maelfu ya waandamanaji walioweka kambi nje ya jengo la serikali.

"Kama hutatusikiliza, tutazidisha maandamano mpaka wewe na familia yote ya Shinawatra mshindwe kutembea. Mtawezaje kutembea wakati watu wakiwatemea mate kila siku?” aliongeza.

Hata hivyo, Yingluck, alipuuza wito wa waandamanaji wa kumtaka ajiuzulu, akiapa kuendelea kuwa waziri mkuu wa mpito mpaka uchaguzi mkuu utakaofanyika Februari 2.

Maandamano ya kuipingia serikali yalianza Oktoba 31 baada ya serikali kuwasilisha bunge muswada ambao ungetoa msamaha kwa Thaksin na kumuwezesha kurejea nchini.

Waandamanaji wanamtuhumu Thaksin kuwa bado anaiendesha nchi kwa mlango wa nyuma, na wameapa kuibomoa nguvu yake katika siasa za nchi hiyo.

Bilionea huyo aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya mwaka 2006, amekuwa akiishi uhamishoni tangu mwaka 2008. Mahakama nchini humo ilimpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela iwapo atarejea Thailand.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment